Sports news

Kocha wa Saudi Arabia akanusha taarifa za wachezaji wake kupewa Rolls Royce

Kocha wa Saudi Arabia akanusha taarifa za wachezaji wake kupewa Rolls Royce

Kocha wa timu ya Taifa ya Saudi Arabia Herve Renard amekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao zikisema kwamba wachezaji wote wa timu hiyo watazawadiwa magari aina ya Rolls Royce kufuatia ushindi wao mkubwa dhidi ya Argentina kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar.

Kwa mujibu wa The New York Post, Herve Renard amesema hakuna ukweli kwenye taarifa hiyo “Hakuna ukweli wowote kuhusu hili. Tuna Shirikisho imara pamoja na Wizara ya Michezo. Na huu sio muda wa kupata chochote. Muhimu zaidi kwetu ni kumaliza 1 au 2 kwenye kundi.” alisema Kocha Renard.

Taarifa hizo za wachezaji kupewa zawadi ya gari aina ya Rolls-Royce na Prince Mohammed Salman, zimekanushwa pia na Mshambuliaji wa timu hiyo, Saleh al-Shehri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *