
Rapa Breeder Lw anaendelea kutupasha kuhusu EP yake mpya ijayo aliyoipa jina la Vibes & Ting.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha kuwa EP hiyo itaingia rasmi sokoni Disemba 2 mwaka 2022 ambapo amewataka mashabiki kukaa mkao wa kula kupokea kazi hiyo ambayo ameitaja kuwa ni ya kitofauti.
Vibes & Tings EP ina jumla ya. Nyimbo 8 za moto ambazo amezifanya mwenyewe bila kumshirikisha msanii yeyote.
Kwa sasa mashabiki wanaweza kui-pre-order EP hiyo kupitia digital platforms mbali mbali za kupakua na kusikiliza muziki duniani ikiwemo Apple Music.