
Mwanamuziki anayekuja kwa kasi nchini Uganda Martha Mukisa ameweka wazi tarehe ambayo ataachia EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Sisaaga.
Hitmaker huyo wa “Sango” amethibitisha kwamba EP yake itaingia sokoni Desemba 9 mwaka huu ikiwa na jumla ya nyimbo saba za moto.
Mukisa amemtaja Oman Rafiki na Liam Voice kama wasanii waliomsaidia kuandika nyimbo zinazopatikana kwenye EP hiyo huku maprodyuza Nessim, Ronnie, Bash killer, na Brian beats ambao wamehusika pakubwa kuiandaa EP hiyo.
Mrembo huyo anaamini kuwa EP hiyo, itamsaidia kupenya kwenye soko la kimataifa kutoka na ubora wake.
Sisaaga EP inaenda kuwa kazi ya kwanza kwa mtu mzima Martha Mukisa tangu aanze safari yake ya muziki miaka kadhaa iliyopita.