Entertainment

Nikita Kering ashindwa kuficha furaha yake kwa kutumbuiza kwenye Afrobeat Concerto ya BBC Radio 1Xtra.

Nikita Kering ashindwa kuficha furaha yake kwa kutumbuiza kwenye Afrobeat Concerto ya BBC Radio 1Xtra.

Msanii Nikita Kering ameshindwa kuficha furaha yake baada ya kutumbuiza katika shoo ya kituo cha habari BBC 1Xtra mwishoni mwa wiki pamoja na baadhi ya wasaniii makubwa ya tasnia ya muziki dunia.

Kupitia ukurasa wake wa instagram amewashukuru mashabiki zak kwa upendo ambapo ameenda mbali Zaidi kuahidi ataendelea kuwapa muziki mzuri

“A dream come true😭✨ @sofresh254 thank you for making this track with me🙏🏾I have so much to learn, can’t wait to see what Better looks like!,” Aliandika.

Mafanikio yake makubwa na kutumbuiza kwenye jukwaa la kimataifa inakuja baada ya kutangazwa kama balozi wa programu ya EQUAL kwa mwezi wa Novemba na mtandao wa kusikiliza muziki  waSpotify.

Mwanamuziki huyo aliyeshinda tuzo na mtunzi wa nyimbo wiki kadhaa zilizopita aliangaziwa kwenye bango la New York Times Square nchini Marekani kwa hisani ya Spotify na pia kabla ya yeye kutumbuiza kwenye sshoo ya Afrobeat Concerto Iliyotayarishwa na kituo cha BBC Radio 1Xtra.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *