
Mwimbaji nyota wa BongoFleva Juma Jux ametangaza kusogeza mbele uzinduzi wa album yake mpya King Of Hearts ambapo sasa uzinduzi huo utafanyika Disemba 7.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Jux ameeleza kwamba amefikia maamuzi hayo ili kuhakikisha wasanii wote walioshiriki kwenye album yake wana perform siku ya uzinduzi ndani ya ‘The Super Dome’ Masaki, Jijini Dar es salaam.
Lakini pia amebainisha kwamba, siku hiyo ya uzinduzi itajawa na surprise kibao na kuweka historia.
“Siku ya tarehe 7 Disemba nataka iwe siku ya Industry nzima kuweka historia. Kuanzia ukumbi ambao itafanyika Show hii, Stage, Mavazi, Performance na kila kitu “, ameeleza Juma Jux.