Entertainment

Pinky afukuzwa Team No Sleep kwa madai ya kuvuta Shisha

Pinky afukuzwa Team No Sleep kwa madai ya kuvuta Shisha

Msanii anayekuja kwa kasi nchini Uganda Pinky ameripotiwa kutimuliwa kwenye lebo ya muziki ya Team No Sleep kwa madai ya kutoka kimapenzi na wanaume tofauti na kuvuta shisha.

Duru za kuaminika zinasema licha ya meneja wake Jeff Kiwa kumuonya kila mara kujitenga na tabia hatarishi itakayomshusha kisanaa, aliendelea kumpuuza, jambo ambalo lilifanya uongozi wa TNS kusitisha mkataba wa kufanya naye kazi.

Pinky mwenye umri wa miaka 18 amekuwa chini ya Jeff Kiwa kwa takriban miaka miwili lakini hana wimbo wowote mkali kwenye maktaba yake ila bado anajitahidi kuwaaminisha mashabiki kuwa ana kipaji cha kipekee katika muziki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *