
Msanii Kelechi Africana amepuzilia mbali tuhuma za kumtelekeza mtoto wake.
Kelechi amesema madai ya kumkimbia mtoto wake hayana msingi wowote ikizingatiwa kuwa amekuwa akitekeleza majukumu yake kama baba.
Hitmaker huyo wa “Nimechoka” amesema baby mama wake anatafuta umaarufu kupitia jina lake kwa kutengeneza lawama ambazo hazina ukweli.
Kauli ya Kelechi inakuja mara baada ya taarifa kusambaa mtandaoni kuwa amefikishwa kwenye mahakama ya watoto ya Tononoka kwa kosa la kumtelekeza mtoto wake.
Awali baby mama wake aitwaye Shinaz Shaz alidai kwamba Kelechi amekuwa akikwepa majukumu yake kama baba, jambo lilomfanya amtumie maafisa wa polisi alipokuwa kwenye show huko Voi mwisho mwa juma lilopita.