Entertainment

Adidas yavunja mkataba na Kanye West

Adidas yavunja mkataba na Kanye West

Kampuni ya Adidas imeripotiwa kuvunja uhusiano wake wa kibiashara na Kanye West kufuatia kauli yake ya chuki dhidi ya Jamii ya Wayahudi.

“Kampuni ya Adidas haivumilii hata kidogo maneno ya chuki na hatarishi kwa Umma yaliyotolewa na Kanye West. Kampuni imeamua kuvunja mkataba na Kanye West pamoja na kusitisha bidhaa zote zilizokuwa na ushirikiano pamoja na Yeezy” Imesomeka sehemu ya taarifa ya Adidas iliyotolewa kwa Umma.

Itakumbukwa, tayari makampuni mengine kama Def Jam Records, Balenciaga na CAA yaliyokuwa yakifanya kazi na Kanye West, yashajiondoa kufanya nae kazi kufuatia sakata hilo la kauli za chuki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *