
Staa wa muziki kutoka DR Congo Fally Ipupa ndiye msanii pekee wa Afrika Mashariki aliyechaguliwa kuwania tuzo za BET 2022 ambazo zinatarajiwa kutolewa Juni 26 mwaka huu nchini Marekani.
Mkali huyo anawania kipengele cha Best International Act akishindana na wasanii kama Fireboy DML na Tems wote kutokea nchini Nigeria.
Utakumbuka mwaka jana mwimbaji wa Bongofleva toka WCB Wasafi Diamond Platnumz ndiye alikuwa msanii pekee wa Afrika Mashariki kwenye tuzo hizo.
Katika hatua nyingine Wizkid ametajwa kwenye vipengele viwili, Best Male R&B/ Pop Artist na Best Collaboration (ft. Tems & Justin Bieber), huku Tems akitajwa tena kwenye kipengele cha Best New Artist.
Upande wa Marekani Mwimbaji Doja Cat ameongoza kwa kutajwa kwenye vipengele vingi zaidi, akitajwa kwenye vipengele sita.