
Akaunti ya Youtube ya mwanamuziki wa mugithi Samidoh imerejeshwa hewani baada ya kufutwa kwa kukiuka sheria za mtandao huo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Samidoh ameshindwa kuficha furaha yake kwa kuchapisha ujumbe wa kumshukuru Mungu kwa kujibu maombi yake na pia kuwataka mashabiki zake waendelee kumuonyesha upendo kupitia kazi zake za muziki.
Kaunti ya youtube ya Samidoh ilifunguliwa rasmi Mei 11 mwaka 2011 na mpaka sasa ina jumla ya watazamaji millioni 47.
Samidoh kwa sasa yupo nchini Marekani kwa ziara ya kimuziki iliyoanza Oktoba 2022 ambapo inatarajiwa kukamilika Disemba 3 mwaka huu.