Entertainment

Akon Ashindwa Kujizuia Baada ya Senegal Kutwaa Ubingwa wa AFCON 2025

Akon Ashindwa Kujizuia Baada ya Senegal Kutwaa Ubingwa wa AFCON 2025

Staa wa muziki duniani Akon alishindwa kujizuia kufuatia ushindi wa kihistoria wa timu ya taifa ya Senegal baada ya kuitandika Morocco kwa bao moja kwa sufuri na kutwaa ubingwa wa AFCON katika mchezo ulioshuhudiwa jana jijini Rabat, Morocco.

Akon, ambaye ana asili ya Senegal, alionekana akiwa na furaha tele mara baada ya filimbi ya mwisho, akiwakumbatia wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Senegal, ishara ya fahari kubwa kwa taifa lake la asili.

Msanii huyo hakusita kutoa pongezi kwa kikosi kizima, akimtaja nyota Sadio Mané kama nguzo muhimu aliyelibeba taifa hilo katika mechi hiyo ngumu.

Akon alikuwa miongoni mwa mastaa kadhaa wa kimataifa wenye asili ya Senegal waliojitokeza kuipa sapoti timu yao, jambo lililoongeza morali kwa wachezaji ndani na nje ya uwanja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *