Akon Ashindwa Kujizuia Baada ya Senegal Kutwaa Ubingwa wa AFCON 2025

Akon Ashindwa Kujizuia Baada ya Senegal Kutwaa Ubingwa wa AFCON 2025

Staa wa muziki duniani Akon alishindwa kujizuia kufuatia ushindi wa kihistoria wa timu ya taifa ya Senegal baada ya kuitandika Morocco kwa bao moja kwa sufuri na kutwaa ubingwa wa AFCON katika mchezo ulioshuhudiwa jana jijini Rabat, Morocco. Akon, ambaye ana asili ya Senegal, alionekana akiwa na furaha tele mara baada ya filimbi ya mwisho, akiwakumbatia wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Senegal, ishara ya fahari kubwa kwa taifa lake la asili. Msanii huyo hakusita kutoa pongezi kwa kikosi kizima, akimtaja nyota Sadio Mané kama nguzo muhimu aliyelibeba taifa hilo katika mechi hiyo ngumu. Akon alikuwa miongoni mwa mastaa kadhaa wa kimataifa wenye asili ya Senegal waliojitokeza kuipa sapoti timu yao, jambo lililoongeza morali kwa wachezaji ndani na nje ya uwanja.

Read More
  Kesi ya Talaka Yaibua Siri za Mali ya Akon

 Kesi ya Talaka Yaibua Siri za Mali ya Akon

Mwimbaji maarufu wa muziki wa R&B, Akon, anakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisheria na kifedha baada ya mke wake, Tomeka Thiam, kufungua rasmi kesi ya talaka baada ya ndoa yao kudumu kwa miaka 29. Kwa mujibu wa taarifa zilizowasilishwa mahakamani, Tomeka anadai euro milioni 100 kama sehemu ya mgawanyo wa mali, akisema kuwa alichangia kwa kiasi kikubwa katika kujenga utajiri na mafanikio ya Akon tangu mwanzo wa safari yake ya muziki. Hata hivyo, ripoti ya awali ya ukaguzi wa mali iliyowasilishwa mahakamani imeibua mshangao baada ya kubaini kuwa Akon ana kiasi cha dola 10,000 pekee kwenye akaunti yake binafsi, huku mali na fedha nyingine zikidaiwa kuwekwa kwa jina la mama yake. Kesi hiyo sasa imezua gumzo kubwa mitandaoni, huku mashabiki na wadau wa muziki wakitilia shaka taarifa hizo za kifedha, wakijiuliza ikiwa msanii huyo ambaye amekuwa akihusishwa na miradi mikubwa ya maendeleo barani Afrika, hasa mradi wa “Akon City” nchini Senegal, kweli amefikia hatua ya kifedha ya namna hiyo. Mahakama inatarajiwa kusikiliza ushahidi zaidi katika wiki zijazo ili kubaini ukweli wa madai hayo na kupanga namna ya kugawa mali kati ya wawili hao.

Read More