LifeStyle

Akothee Akimbizwa Hospitalini Baada ya Maumivu Makali ya Tumbo

Akothee Akimbizwa Hospitalini Baada ya Maumivu Makali ya Tumbo

Mwanamuziki kutoka Kenya, Akothee, amefichua tukio la kutisha alilopitia alfajiri ya jana baada ya kuanguka chooni kutokana na maumivu makali ya tumbo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Akothee amesema kuwa hali hiyo ilianza usiku wa manane baada ya kushuhudia video ya kutisha ya msichana aliyekuwa nyumbani kwake. Amesema tukio hilo lilimshtua kiasi cha kumsababishia maumivu makali, kutapika, kuharisha, na hisia za woga ambazo zilimfanya kushindwa hata kulala.

Akothee ameeleza kuwa maumivu yalimfanya kulala ndani ya choo kwa kujaribu kupunguza hali hiyo. Amesema kufikia saa tisa asubuhi, nguvu zake zilimwishia na akaanguka sakafuni huku akijaribu kufika chumbani kwa watoto wake akiwa analia kwa maumivu makali.

Mwanamama huyo amesema watoto wake walimpata akiwa amelala chooni na mara moja walimkimbiza hospitalini kupitia kitengo cha dharura. Amedai familia yake ilikabiliana na changamoto ya kupokea matibabu haraka baada ya muuguzi kuonyesha ukatili na kutokuwa na huruma.

Hata hivyo Akothee amesema baada ya jitihada hizo, hatimaye alipatiwa matibabu na sasa anaendelea kupona, ingawa tukio hilo limemuacha akiwa na hofu kubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *