Entertainment

Akothee amuombea msamaha kwa Mungu shabiki aliyemuombea mabaya

Akothee amuombea msamaha kwa Mungu shabiki aliyemuombea mabaya

Msanii na mfanyibiashara tajika Akothee amezua gumzo mtandaoni baada ya kumjibu Shabiki kwenye post yake.

Akothee kwenye mtandao wake wa kijamii alipost picha akiwa mjamzito lakini Shabiki Kwa jina Mercy Joe aliandika kwenye komenti akiombea ujauzito huo upotee.

Jambo ambalo limeleta hisia chungu nzima huku Akothee akimjibu na kukwambia maombi yake yalijibiwa na alipoteza ujauzito huo.

Hata hivyo amemalizia kwa kumuombea msamaha kwa Mungu shabiki huyo aliyeuombea ujauzito wake mabaya.

Baadhi ya wakenya wameonekana kumhurumia Akothee huku wengine wakimshambulia shabiki huyo kwa kumtakia maneno mabaya mwimbaji huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *