
Mwanamuziki asiyeishiwa na vituko kila leo nchini Akothee amezua ngumzo mtandaoni mara baada ya kudai kwamba wanawake wengi ambao hawaposti wapenzi wao kwenye mitandao ya kijamii wapo kwenye mahusiano mengine.
Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Akothee amesema wanawake sampuli hiyo wanashiriki vitendo vya usaliti kwa kutoka kimapenzi na wanaume tofauti ambao mara nyingi huwatimizia mahitaji yao ya msingi, jambo amedai limewafanya kusahau kuwaonyesha upendo wapenzi wao.
Hata hivyo ujumbe huo wa Akothee umezua hisia kinzani kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo baadhi wamekubaliana nae huku wengine wakionekana kushangazwa na kauli ya mwanamama huyo ambaye amekuwa kwenye mahusiano mengi ya kimapenzi na wanaume mbali mbali.
Kauli ya Akothee inakuja siku chache mara baada ya kumtambulisha mpenzi wake mzungu na kudai kuwa yuko tayari kufunga nae ndoa kwa kuwa ameshapata furaha ambayo amekuwa akitafuta kwa muda mrefu.