
Siku chache baada ya Mwanamitido wa urembo nchini Dennis Karuri kudai Akothee ndiye mteja mkorofi zaidi kuwahi kufanya naye kazi, shutuma nyingine imeibuliwa dhidi ya mwanamuziki huyo.
Mfanyakazi wake wa zamani aliyefahamika kwa jina la Brenda amejitokeza na kudai kuwa Akothee amekataa kumlipa mshahara wake wa shillingi Sh60,000 licha ya kumfanyia kazi ya kushoot video kwenye shughuli zake kwa miezi miwili.
Brenda amemtaja akothee kama mtu katili asiyekuwa na uhuruma ambapo ametishia kumchukulia hatua kali za kisheria msanii huyo kwa kutothamini kazi aliyomfanyia.
Hata hivyo, akothee amejibu tuhuma hizo kwa kusema kuwa mlalamishi alifeli kutekeleza majukumu yake ipasavyo, hivyo hangelipwa kwa kazi ambayo hakufanya huku akitishia kumchukulia Brenda hatua za kisheria akisema hatakubali jina lake lichafuliwa na mtu yeyote.