
Staa wa muziki nchini Akothee ametishia kuwachukulia hatua kali za kisheria wanablogu wanaotumia maudhui anayochapisha kwenye mitandao yake ya kijamii.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema anapania kuzifungulia kesi blogu hizo kwa kutumia maudhui yake bila ridhaa yake huku akisisitiza kuwa huenda akawatoza faini ya shillingi millioni 300 ili iwe funzo kwao wanapoandika habari zisizo na uhakika.
Mama huyo wa watoto 5 amesema wanablogu mara nyingi wamekuwa wakipendelea kuchapisha taarifa hasi dhidi yake badala ya kumsaidia kukuza biashara yake.
Akothee amewatolea uvivu wanablogu wa kenya akiwataja kama watu wasiokuwa na kipato ambao wamekuwa na mazoea ya kujificha nyuma kompyuta kumharibia brand au chapa yake ya muziki.