
Album ya msanii Harmonize, “Afro East” imefikisha jumla ya Streams millioni 15 kwenye mtandao wa Audiomack.
Album hiyo ya kwanza kwa mtu mzima Harmonize iliachiwa rasmi Machi 14, mwaka 2020 ikiwa na jumla ya ngoma 17 za moto.
Aidha, Boss huyo wa Konde Gang mapema mwezi huu alitangaza kuachia album yake mpya na ya tatu mwezi Juni. Ikumbukwe album yake ya pili ambayo ni “High School” ilitoka Novemba 5, mwaka 2021.
Huu unakuwa ni muendelezo wa Harmonize kuachia ngoma mfululizo bila kupoa huku namba zikiendelea kuwa nzuri pia kupitia akaunti zake za digital platforms.