
Album ya msanii Mbosso, “Definition Of Love” inaendelea kufanya vizuri kwenye digital platforms mbalimbali.
Good news ni kwamba tayari imefikisha jumla ya Streams MILIONI 55 kwenye mtandao wa Boomplay.
“Definition Of Love”, ndio album ya kwanza kwa mtu mzima Mbosso kuiachia tangu aanze safari yake ya muziki na pia alipojiunga na lebo ya WCB mwaka 2018.
Album ya “Definition Of Love”, iliachiwa rasmi Machi 9, mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya nyimbo 12 za moto zenye maudhui ya mapenzi.