Entertainment

ALBUM YA MBOSSO “DEFINITION OF LOVE” YAWEKA REKODI KWENYE DIGITAL PLATFORMS MBALI MBALI

ALBUM YA MBOSSO “DEFINITION OF LOVE” YAWEKA REKODI KWENYE DIGITAL PLATFORMS MBALI MBALI

Hatimaye albamu ya mwanamuziki wa Bongofleva, Mbosso ‘Definition of Love’ imefanikiwa kufikisha streams zaidi ya Milioni 150.

Albamu hiyo ilitoka Machi 9, mwaka 2021 ikiwa na njimbo 12 ambazo ameshirikiana na wasanii zaidi ya nane kutoka Tanzania, Uganda na Nigeria,

Streams hizo milioni 150 ni jumla ya streams zote kutoka kwenye mitandao yote iliyowekwa albamu hiyo tangu itoke rasmi.

Utakumbuka Mbosso anakuwa msanii wa kwanza kuachia albamu miongoni mwa wale waliokuwa wanaunda kundi la Yamoto Band chini ya Mkubwa na Wanawe.

Mbosso aliyejiunga na WCB Wasafi Januari 28, mwaka wa 2018 alikuwa kwenye kundi hilo na Aslay, Beka Flavour na Enock Bella ambao hadi sasa hawajatoa albamu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *