Entertainment

Album ya Mbuzi gang yafikisha streams zaidi ya milioni 1 Boomplay

Album ya Mbuzi gang yafikisha streams zaidi ya milioni 1 Boomplay

Album ya kundi la muziki nchini, Mbuzi Gang “Three Wise Goats” inaendelea kubadilisha namba kila leo kwenye digital platforms mbalimbali.

Habari njema ni kwamba tayari imefikisha jumla ya Streams Milioni moja kwenye mtandao wa Boomplay ndani ya mwaka mmoja tangu itoke rasmi.

Album hiyo ambayo ina jumla ya nyimbo 13 za moto,iliachiwa rasmi mwezi Januari mwaka 2022 ikiwa na kolabo 10 pekee kutoka kwa wakali kama Jose Chameleone, Lava Lava,KRG The Don, Nina Roz, Katapilla, Ethic, Madini Classic, Naiboi na wengine kibao.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram Mbuzi Gang wamewashukuru mashabiki zao kwa upendo kwa kuandika, “1 million Streams on this masterpiece. Thank you fam. #3WG

Ikumbukwe “Three Wise Goats” ni Album ya kwanza kwa kundi la Mbuzi Gang ambalo linaundwa na wasanii watatu ambao ni Fathermoh, Joefes na iphoolish.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *