Entertainment

Ali Kiba Aomba Msamaha Watanzania kwa Kujihusisha na Siasa

Ali Kiba Aomba Msamaha Watanzania kwa Kujihusisha na Siasa

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva Alikiba ameomba radhi kwa Watanzania kufuatia hasira zilizozuka baada ya yeye kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa kampeni za uchaguzi wa hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alikiba amewaomba radhi Watanzania kwa kuwaumiza kupitia msimamo wake wa kisiasa na kuwapa pole wale wote waliopoteza maisha au kujeruhiwa wakati wa machafuko yaliyoshuhudiwa baada ya uchaguzi, wakiwa wanaitetea nchi yao.

Kauli yake imekuja wakati ambapo wananchi wengi nchini Tanzania wamekuwa wakikosoa baadhi ya wasanii wakubwa nchini humo waliounga mkono serikali ya Rais Samia Suluhu iliyopewa lawama kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.

Hata hivyo, wafuasi wengi mtandaoni wamesema msamaha huo umechelewa, lakini ni hatua muhimu katika kuponya majeraha ya kijamii yaliyosababishwa na siasa zenye mgawanyiko nchini Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *