Entertainment

ALI KIBA ATANGAZA UJIO WA ZIARA YAKE YA MUZIKI

ALI KIBA ATANGAZA UJIO WA ZIARA YAKE YA MUZIKI

Staa wa muziki wa Bongofleva Ali Kiba ametangaza rasmi ujio wa ziara yake kimuziki ya kimatifa inayokwenda kwa jina la “Only One King”

Boss huyo wa King’s Music ametangaza ujio huo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema ataanzia tour hiyo nchini Marekani, Septemba mwaka huu.

Ali Kiba amesema, ana miaka takribani minne hajafanya ziara ya kimuziki nchini Marekani, hivyo sasa ni wakati wa kukutana na mashabiki wake wa huko.

“Let the International Tours begin!! And my first tour will be in USA !!! It’s been 4 years since I was in the united states to connect with my fans, i would like to officially announce I will be starting my USA Tour this September” ameeleza ALIKIBA kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Hata hivyo ameeleza hivi karibuni ataweka wazi tarehe na mahala atakapofanya ziara hiyo nchini Marekani.

“Tour dates will be announced soon be ready to party and be entertained. For Bookings & Inquires please Call 323.868.6114” – ALIKIBA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *