Entertainment

Ali Kiba awashauri wasanii kuzingatia maadili mema kwenye utayarishaji wa kazi zao

Ali Kiba awashauri wasanii kuzingatia maadili mema kwenye utayarishaji wa kazi zao

Mwimbaji wa Bongofleva Ali kiba amekosoa baadhi ya wasanii kuimba na kufanya video zisizo na maadili ambazo zinaharibu jamii hasa watoto.

Kwenye mahojiano yake na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya America (VOA), Boss huyo wa King’s Music pia ametoa ushauri kwa wanamuziki kulinda maadili ya jamii kwa kuzingatia malezi hasa ya vijana ambao hivi leo dunia imekuwa kama kijiji na matendo yote ya wanamuziki yanashuhudiwa mubashara kupitia mitandao ya kijamii na vijana hao.

Ali Kiba kwa sasa yupo nchini Marekani kwenye ziara yake ya Kimuziki, na Jumamosi hii tarehe 12 anatarajia kufanya show yake ya kwanza huko Louiseville, Kentucky.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *