
Mastaa wa Muziki wa Bongofleva Ali Kiba na Shilole wamethibitisha kumaliza tofauti zao.
Wawili hao wameonesha kumaliza tofauti zao Mkoani Kigoma nchini tanzania mbele ya Mashabiki Baada ya alikiba kumpandisha jukwaani Shilole na Kuthibitisha kuwa hawana utofauti.
Kwenye video Shilole anaseema “Tunaishi kwa kusapotiana, Alikiba namkubali, ila twende tukawatoe watu utata ulisema hukunialika na Alikiba alikubali kwamba amemualika”.
Kutokuelewana kwao kulianza Mwaka jana mwezi Oktoba mara baada ya Ali Kiba kumkataa Shilole kuwa hakumualika kwenye Hafla yake ya Uzinduzi wa Album ya ONLY ONE KING licha ya kuwa Shilole Aliudhuria katika hafla hiyo.