Entertainment

Alien Skin Atangaza Kuacha Muziki Kufuatia Kesi ya Mauaji

Alien Skin Atangaza Kuacha Muziki Kufuatia Kesi ya Mauaji

Msanii mwenye utata kutoka Uganda, Alien Skin, amewashangaza mashabiki na wadau wa muziki baada ya kutangaza kujiondoa rasmi kwenye tasnia ya muziki kupitia TikTok Live.

Alien Skin, ambaye ni bosi wa Fangone Forest boss, amesema amechoka na upinzani mkubwa anaoupata kutoka kwa wasanii wenzake na hata mashabiki, akifafanua kuwa hali hiyo imemuweka kwenye mawazo na msongo wa akili.

Msanii huyo ambaye amekuwa kwenye sanaa kwa takriban miaka minne, amesema maadui zake wanajitahidi kila njia kumchafua, na kwa sababu hiyo ameamua kuacha muziki na kujikita kwenye maisha ya faragha

Tangazo hilo limekuja wakati nyota huyo anakabiliwa na tuhuma nzito za mauaji. Jeshi la Polisi la Kampala Metropolitan limethibitisha kuwa linamchunguza Alien Skin na washirika wake kwa madai ya kuhusika katika kifo cha dansa Wilfred Namuwaya, maarufu Top Dancer. Inadaiwa kuwa Namuwaya alipigwa na kundi la washirika wa msanii huyo, hali iliyomsababishia matatizo ya kiafya na hatimaye kupelekea kifo chake mapema wiki hii.

Msemaji wa Polisi, Patrick Onyango, amesema uchunguzi unaendelea na Alien Skin ndiye mtuhumiwa mkuu. Iwapo atapatikana na hatia ya kosa hilo la mauaji, anaweza kukabiliwa na kifungo cha maisha gerezani au hata adhabu ya kifo chini ya sheria za Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *