Alien Skin Atoa Onyo Kali kwa Wafuasi wa NUP

Alien Skin Atoa Onyo Kali kwa Wafuasi wa NUP

Msanii mwenye utata nchini Uganda, Alien Skin, ametoa onyo kali kwa wafuasi wa chama cha National Unity Platform (NUP) akiwataka waache kumshambulia mitandaoni. Akizungumza kupitia TikTok Live, Alien Skin amesema kuwa yuko kwenye level moja na kiongozi wa chama hicho, Bobi Wine ikizingatiwa kuwa ana ushawishi mkubwa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii. Msanii huyo amesisitiza kuwa anastahili heshima, kutambuliwa na kuungwa mkono kama ilivyo kwa Bobi Wine, akieleza kuwa ana wafuasi wengi na nguvu ya kuwavuta vijana katika maeneo mbalimbali ya Uganda. Kwa takribani miaka miwili sasa, Alien Skin amekuwa katika mvutano wa mara kwa mara na wafuasi NUP, hali iliyojaa maneno makali na mabishano kwenye majukwaa mbalimbali ya kijamii. Inadaiwa kuwa mzozo huo ulianza baada ya msanii huyo kujitenga na kambi ya upinzani na kuonyesha wazi kumuunga mkono chama tawala cha NRM, hatua iliyowakasirisha pakubwa wafuasi wengi wa NUP.

Read More
 Museveni Amshauri Alien Skin Aachane na Muziki Kama Umemshinda

Museveni Amshauri Alien Skin Aachane na Muziki Kama Umemshinda

Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, amempa onyo kali msanii mwenye utata Alien Skin baada ya msanii huyo kuonekana hadharani akipinga baadhi ya sera za serikali kupitia muziki na majukwaa yake ya mitandao ya kijamii. Akizungumza na msanii huyo kwenye ikulu jijini Kampala, amemshauri msanii huyo kama anaona muziki unamlemea au hauendani na dhamira ya kujenga jamii, basi ni busara kwake kuachana nao mapema. Rais huyo amemuelekeza Alien Skin kujikita katika shughuli nyingine za kujitegemea kama kilimo, akisema sekta hiyo ina mchango mkubwa katika uchumi wa taifa na haina migongano kama ile inayojitokeza kwenye muziki wenye ujumbe tata. Rais Museveni ameonya kuwa kutumia sanaa kama jukwaa la kupinga juhudi za maendeleo ni sawa na kuwa kikwazo kwa mustakabali wa taifa. Amewataka wasanii kutumia vipaji vyao kuhimiza umoja, uzalendo na maendeleo ya taifa badala ya kueneza ujumbe unaoweza kuwagawanya vijana au kuchochea chuki dhidi ya serikali.

Read More
 Alien Skin Awashutumu Wasanii Wanaoshiriki Kampeni za Museveni

Alien Skin Awashutumu Wasanii Wanaoshiriki Kampeni za Museveni

Msanii mwenye utata mkubwa nchini Uganda, Alien Skin, ametoa matamshi makali dhidi ya wasanii wanaoendelea kutumbuiza kwenye kampeni za Rais Yoweri Museveni baada ya kujiondoa kwenye misafara ya kampeni kutokana na malipo duni. Akiwa jijini Kampala, Alien Skin amewakashifu wasanii hao, akisema juhudi zao hazina nguvu kwa sababu muziki wake ndio unaoamsha umati na kuongeza hamasa kwenye mikutano ya kisiasa. Anadai kuwa hata akiwa hayupo kwenye eneo la kampeni, nyimbo zake ndizo zinazoongoza na kutawala hewani, hali inayochangia kuvutia wafuasi wengi. Alien Skin anasema kwa msingi huo, anapaswa kulipwa kwani muziki wake ndio unaotumika kuongeza namba za watu kwenye kampeni na kuleta nguvu kwenye mikutano hiyo. Kauli hizi zinakuja siku chache baada ya video kusambaa mtandaoni ikimuonyesha Eddy Kenzo na wasanii wengine wakicheza wimbo wa Alien Skin katika mkutano wa Museveni huko mashariki mwa Uganda, huku Alien Skin mwenyewe akiwa hajahudhuria.

Read More
 Msanii Alien Skin Anusurika Kifo Baada ya Kushambuliwa Jinja

Msanii Alien Skin Anusurika Kifo Baada ya Kushambuliwa Jinja

Msanii mwenye utata kutoka Uganda, Alien Skin, amenusurika kifo baada ya kushambuliwa na kundi la vijana wakorofi wakati wa ziara yake katika mji wa Jinja siku ya Alhamisi. Mkali huyo wa ngoma ya Sitya Danger alikuwa amesafiri hadi mji huo kwa ajili ya kutumbuiza katika mkutano wa kisiasa wa chama cha NRM, lakini hali ilibadilika ghafla na vurugu kuzuka muda mfupi baada ya onyesho lake kumalizika. Mashuhuda wanasema kuwa baadhi ya vijana waliokuwa kwenye umati waligeuka wenye fujo, jambo lililowalazimu polisi na waandaaji wa hafla hiyo kuingilia kati haraka kumwokoa msanii huyo. Alien Skin aliondolewa kwa dharura na kikosi chake cha usalama hadi sehemu salama. Duru za kuaminika zinasema kuwa huenda tukio hilo lilichochewa na mivutano ya kisiasa, ikizingatiwa kuwa msanii huyo amewahi kutofautiana na wafuasi wa chama cha upinzani cha National Unity Platform (NUP) kinachoongozwa na Bobi Wine, ambaye ana ushawishi mkubwa katika eneo hilo. Hii si mara ya kwanza kwa Alien Skin kukumbwa na vurugu katika eneo la mashariki mwa Uganda, mapema mwaka huu aliripotiwa kushambuliwa mjini Iganga baada ya onyesho jingine.

Read More
 Polisi Uganda Wakanusha Kumkamata Alien Skin

Polisi Uganda Wakanusha Kumkamata Alien Skin

Polisi nchini Uganda wamekanusha taarifa zilizodai kwamba msanii mwenye utata Alien Skin amekamatwa kwa tuhuma za mauaji. Kupitia msemaji wa Polisi wa Kanda ya Kampala, imeelezwa kwamba msanii huyo hajakamatwa na hayupo mikononi mwao, lakini anasakwa na vyombo vya dola. Polisi wamewataka wananchi kutoa taarifa iwapo kuna mtu yeyote anayefahamu alipo, kwa kuwa msanii huyo yupo kwenye orodha ya wahalifu wanaotafutwa. Kauli ya Polisi inakuja siku chache baada ya mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii kusambaza taarifa kwamba bosi huyo wa Fangone Forest amekamatwa na kutupwa rumande kwa makosa mbalimbali ikiwemo mauji ya dansa maarufu wa Kampala, ambaye alizikwa wiki iliyopita katika Wilaya ya Mbale.

Read More
 Msanii wa Uganda Alien Skin Adaiwa Kukamatwa kwa Tu­huma za Mauaji

Msanii wa Uganda Alien Skin Adaiwa Kukamatwa kwa Tu­huma za Mauaji

Msanii mwenye utata kutoka Uganda, Alien Skin, ameripotiwa kuwekwa kizuizini baada ya kukamatwa mwishoni mwa juma kwa tuhuma za mauaji. Taarifa zinaeleza kuwa msanii huyo, ambaye ni bosi wa Fangone Forest, alinaswa na kikosi cha pamoja cha jeshi na polisi kilichozingira nyumba yake Jumamosi jioni. Inadaiwa kuwa katika upekuzi huo, maafisa wa usalama walikuta mapanga, upinde na mishale pamoja na silaha nyingine hatari nyumbani kwake, jambo lililoibua maswali zaidi kuhusu shughuli zake. Hata hivyo, vyombo vya usalama Uganda ikiwemo polisi na jeshi bado havijathibitisha rasmi kukamatwa kwake. Pamoja na hali hiyo, mashabiki wake wameanzisha kampeni mitandaoni wakitaka aachiliwe mara moja. Kwa mujibu wa mashabiki wake mitandaoni, kukamatwa kwake imehusishwa zaidi na kifo cha dansa mmoja maarufu wa Kampala ambaye alizikwa wiki iliyopita katika wilaya ya Mbale. Mashabiki wake wanadai msanii huyo ametupiwa lawama bila ushahidi wa moja kwa moja. Wakati huohuo, watumiaji kadhaa wa mitandao wamedai kuwa taarifa za kukamatwa kwake si za kweli, wakisisitiza kuwa Alien Skin yupo mafichoni na hajawahi kutiwa mbaroni. Madai ya kukamatwa kwa Alien Skin yameibuka saa chache tu baada ya Naibu Waziri wa Vijana nchini humo kuonya kuwa wasanii wanaoshirikiana na magenge ya kihalifu wako chini ya uchunguzi kwa makosa mbalimbali ikiwemo mauaji.

Read More
 Alien Skin Atangaza Kuacha Muziki Kufuatia Kesi ya Mauaji

Alien Skin Atangaza Kuacha Muziki Kufuatia Kesi ya Mauaji

Msanii mwenye utata kutoka Uganda, Alien Skin, amewashangaza mashabiki na wadau wa muziki baada ya kutangaza kujiondoa rasmi kwenye tasnia ya muziki kupitia TikTok Live. Alien Skin, ambaye ni bosi wa Fangone Forest boss, amesema amechoka na upinzani mkubwa anaoupata kutoka kwa wasanii wenzake na hata mashabiki, akifafanua kuwa hali hiyo imemuweka kwenye mawazo na msongo wa akili. Msanii huyo ambaye amekuwa kwenye sanaa kwa takriban miaka minne, amesema maadui zake wanajitahidi kila njia kumchafua, na kwa sababu hiyo ameamua kuacha muziki na kujikita kwenye maisha ya faragha Tangazo hilo limekuja wakati nyota huyo anakabiliwa na tuhuma nzito za mauaji. Jeshi la Polisi la Kampala Metropolitan limethibitisha kuwa linamchunguza Alien Skin na washirika wake kwa madai ya kuhusika katika kifo cha dansa Wilfred Namuwaya, maarufu Top Dancer. Inadaiwa kuwa Namuwaya alipigwa na kundi la washirika wa msanii huyo, hali iliyomsababishia matatizo ya kiafya na hatimaye kupelekea kifo chake mapema wiki hii. Msemaji wa Polisi, Patrick Onyango, amesema uchunguzi unaendelea na Alien Skin ndiye mtuhumiwa mkuu. Iwapo atapatikana na hatia ya kosa hilo la mauaji, anaweza kukabiliwa na kifungo cha maisha gerezani au hata adhabu ya kifo chini ya sheria za Uganda.

Read More