Gossip

Alikiba Aibua Taharuki Baada ya Kupost Picha ya Zamani Akiwa na Diamond Platnumz

Alikiba Aibua Taharuki Baada ya Kupost Picha ya Zamani Akiwa na Diamond Platnumz

Staa wa muziki kutoka Tanzania, Alikiba, amezua gumzo kubwa mtandaoni baada ya kupakia picha ya zamani akiwa pamoja na mpinzani wake wa muda mrefu, Diamond Platnumz, kupitia ukurasa wake wa Snapchat.

Kitendo hicho kimewasha moto wa mijadala mitandaoni, kwa sababu wawili hao wamekuwa wakitajwa kuwa na uhasama wa muda mrefu ndani ya tasnia ya Bongo Fleva. Mashabiki wengi wameonekana kushangazwa na hatua hiyo, huku wengine wakihisi kwamba huenda tofauti zao tayari zimewekwa pembeni.

Picha hiyo imefungua mlango wa tetesi mpya, baadhi ya mashabiki wakijiuliza kama wakati umefika kwa Alikiba na Diamond kufanya collabo ya pamoja, jambo ambalo limekuwa likisubiriwa kwa hamu kwa miaka mingi. Wadau wa muziki wanasema kitendo hicho ni ishara kwamba huenda upepo mpya unavuma katika tasnia, na inawezekana wawili hao wako kwenye hatua ya kurudisha mahusiano mazuri kikazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *