
Msanii Allan Hendrik ameahidi kuanika siri nzito kuhusu baba mzazi wa King Saha iwapo hatoacha kumshambulia baba yake Bebe Cool.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Hendrick amesema amefanya utafiti na amegundua baadhi ya maovu ambayo baba mzazi wa king saha anajihusisha nayo.
Msanii huyo amesema atamuaibisha King Saha akikataa kumtukana bebe cool licha ya baba yake huyo kumpuza kwa muda kwa muda.
“I have done my research and discovered some dirty things about his father. I’ll go personal if he refuses to chill my dad. He keeps attacking him despite of ignoring him,” amesema Hendrik.
Allan Hendrik tayari ameshaachia nyimbo mbili mbili zinazomtolea uvivu King Saha ambaye amekuwa akimshambulia Bebe Cool kwenye mahojiano mbali mbali.
Utakumbuka juzi kati Bebe Cool alimpa ruhusa mwanae huyo apambane na wanaomkosoa kwenye mitandao ya kijamii.