Gossip

Allan Skin Atuhumiwa Kupora Mazao ya Kasisi Uganda

Allan Skin Atuhumiwa Kupora Mazao ya Kasisi Uganda

Msanii mwenye utata kutoka Uganda, Alien Skin, anakabiliwa na tuhuma nzito za wizi baada ya kasisi maarufu wa jiji la Kampala, Martin Ssempa, kudai kuwa alihusika katika uporaji wa mazao yake ya shambani.

Kwa mujibu wa Ssempa, msafara unaodaiwa kuwa wa Allan ulisimamisha gari la mmoja wa mfanyakazi wake katika barabara ya Nakawuka-Natete,na kisha kumshushia kichapo kikali kabla ya mazao yote kuporwa.

Kasisi Ssempa amesema tukio hilo limekuwa pigo kubwa kwake, kwani mazao hayo yalitarajiwa kusaidia familia yake pamoja na shughuli za kijamii za kanisa. Ametoa makataa ya siku mbili kwa Allan Skin kurejesha mazao hayo, akionya kuwa iwapo hatatii agizo hilo, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Hata hivyo Ssempa amesisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba vitendo vya kupora mali ya wengine haviwezi kuvumiliwa katika jamii.

Tukio hilo linaripotiwa kutokea usiku wa manane mapema wiki hii, wakati mfanyakazi wa kasisi huyo alipokuwa akisafirisha mzigo wa maharagwe na viazi kutoka Kabale kuelekea nyumbani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *