
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu ameweka wazi changamoto anazozipitia katika mahusiano yake ikiwa ni pamoja na kupigwa na kutishiwa kuuawa.
Kupitia instastory yake mrembo huyo ameandika ujumbe mrefu wa masikitiko akieleza namna alivyoumizwa vibaya kwa kipigo huku akidai sababu kubwa ya kupitia manyanyaso hayo ni mtoto wake.
“Daa nimekuwa mtu wakuangaika na kuteseka pasipo sababu ya msingi. Kuna muda natamani kumkumbatia mwanangu nishinde nae nashindwa ‘coz’ nisipo hangaika mwanangu atakula nini?..Nyumba nalipa nini? Leo napigwa kama mbwa kisa kumuhangaikia Mwanangu naumia sahivi mtu ananitishia kuniuaa Mungu”…Aliandika.