Gossip

Amber Ray Afungua Ukurasa Mpya wa Maisha kwa Gari Jipya

Amber Ray Afungua Ukurasa Mpya wa Maisha kwa Gari Jipya

Mrembo maarufu mitandaoni nchini Kenya, Amber Ray, ameendelea kuthibitisha kwamba anajua kujitunza kwa jasho lake baada ya kujizawadia gari jipya la kifahari aina ya Range Rover.

Kupitia ukurasa wake wa Insta Story, Amber alishiriki video na picha zikionyesha mchakato mzima wa gari hilo kusafirishwa kutoka bandarini hadi nyumbani kwake, ambapo ilipokelewa kwa shangwe na familia yake.

Tukio hilo limejiri huku tetesi za kuvunjika kwa uhusiano wake na baba wa mtoto wake, Kennedy Rapudo, zikizidi kushika kasi. Hii ni baada ya Amber kuonekana mara kadhaa kwenye shughuli mbalimbali akiwa peke yake, hali iliyozua gumzo miongoni mwa mashabiki na wafuasi wake mitandaoni.

Hata hivyo, Amber Ray hajazungumzia hadharani kuhusu uvumi huo, akionekana kuzingatia zaidi furaha na mafanikio yake binafsi. Gari hilo jipya limechukuliwa na wengi kama ishara ya kujipenda na kujiendeleza, licha ya changamoto za maisha ya mahusiano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *