
Mrembo kutoka Kenya Anerlisa ambaye alikuwa mke wa msanii wa Bongofleva Ben Pol ameonyesha kutofurahishwa na kile ambacho alikizungumza Ben Pol kwenye mahojiano yake na Ayo Tv kuwa hajawahi kufurahishwa na ndoa yake na mrembo huyo.
Kupitia InstaStory yake anashangaa ni kwanini Ben Pol kila siku amekuwa akiongea mambo mengi ili aonekane mbaya mbele ya umma.
“Ben naona umenizoea na unachukulia ukimya wangu kama udhaifu wangu. Ulikuwa na uwezo wa kumwambia anaekuhoji asikuulize kuhusu mimi. Kwa nini unapenda kila mara mimi nionekane mbaya. Chini ya kapeti unanitumia jumbe tofauti tofauti na namna unavyoniongelea”, Aliandika.
Lakini pia amemtaka Ben Pol aache kumuongelea kwani yeye pia ana mengi kumuhusu lakini amechagua kukaa kimya kama mwanamke.
“Kama kweli wewe ni mwanaume, nakuomba uweke wazi jumbe zote ulizokuwa unanitumia tangu Desemba 25 hadi Januari 4, 2023. Nina mengi ya kuzungumza kuhusu wewe au kuonyesha, lakini nimechagua kusimama kama Mwanamke.” , Aliandika.