
Mwanamuziki kutoka nchini Benin, Angelique Kidjo ameibuka mshindi wa kipengele cha Best Global Music Album kwenye Tuzo za Grammy ambazo zimetolewa usiku wa kuamkia leo.
Kidjo na album yake ‘Mother Nature’ amemuangusha Wizkid kupitia album yake ‘Made In Lagos: Deluxe Edition’ ambayo ilikuwa inapewa kipaumbele.
Lakini pia Wizkid amepata pigo nyingine baada ya mwanamuziki Arooj Aftab kutoka Pakistan kumshinda kwenye kipengele cha best global music performance kupitia ngoma yake ya mohabbat.
Arooj Aftab amewashinda wikzkid kupitia ngoma yake ya Essence, na Burna boy kupitia wimbo wake wa Do Youself aliyomshirikisha Angelique kidjo pamoja.
Utakumbuka Wizkid alitajwa kuwania tuzo za grammy mwaka wa 2022 kupitia vipengele viwili ambavyo ni Best Global Music Perfomance kupitia ngoma ya Essence na Best Global Music Album kupitia album yake ya Made In Lagos: Deluxe Edition.