
Hatimaye mwanamuziki Anjella ameaga rasmi kwa waliokuwa waajiri wake lebo ya muziki Konde Music Worldwide
Nyota huyo amewashukuru Konde Gang kwa kukiona kipaji chake na kumpa nafasi iliyochangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wake kisanaa,
Anjella ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kutuma salamu hizo, ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa taratibu zote za kisheria kuondoka ndani ya lebo hiyo inayoongozwa na msanii Harmonize
Sasa ni rasmi Anjella yupo huru kufanya kazi nje ya lebo hiyo
Harmonize ndiye aliyeanza kutangaza kuachana na mwimbaji huyo kwenye lebo yake, ambapo aliweka wazi hilo Novemba 5, 2022 akithibitisha tetesi zilizokuwa zikienea kuachana nae.
Ikumbukwe, Anjella anakuwa mwanamuziki wa NNE kuachana na Konde Gang ndani ya kipindi kifupi baada ya Country Boy, Cheed na Killy kuachana na lebo hiyo.