Tech news

App ya Threads Yazidi Kukimbiza X/Twitter Kwenye Soko la Mitandao

App ya Threads Yazidi Kukimbiza X/Twitter Kwenye Soko la Mitandao

App mpya ya mitandao ya kijamii, Threads, imetoa ripoti mpya ikionesha kuwa sasa ina watumiaji zaidi ya milioni 400, ikizidi kuimarisha nafasi yake kama mshindani mkubwa wa app ya X (awali Twitter).

Threads, ambayo ni mradi wa kampuni ya Meta, ilizinduliwa kwa lengo la kushindana moja kwa moja na X/Twitter. Kwa kasi kubwa ya ukuaji wake, app hii imeanza kuikimbiza X/Twitter, ambayo kwa sasa ina takriban watumiaji milioni 600 duniani kote.

Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni, ndani ya miezi mitatu tu, Threads imeongeza watumiaji milioni 50, na kwa kasi hii, inatarajiwa kuifikia na hata kuipita X/Twitter katika muda wa mwaka mmoja ijayo.

Hali hii inathibitisha jinsi Threads inavyovutia watumiaji wengi duniani, huku ikionyesha mwelekeo wa kuvunja mipaka ya mitandao ya kijamii na kubadilisha taswira ya mawasiliano mtandaoni.

Watumiaji wengi wanashangazwa na kasi ya ukuaji wa Threads na kuibuka kama jukwaa jipya lenye mvuto mkubwa, hali inayowafanya wataalamu wa teknolojia na masoko kufuatilia kwa karibu mwenendo huu wa soko

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *