Tech news

Apple Yasogeza Uzinduzi wa iPhone 18 Hadi Mwaka 2027

Apple Yasogeza Uzinduzi wa iPhone 18 Hadi Mwaka 2027

Kampuni ya teknolojia ya Apple imetangaza kuwa haitatoa toleo jipya la iPhone 18 mwaka 2026 kama ilivyokuwa ikitarajiwa, bali uzinduzi huo utafanyika mapema mwaka 2027.

Kupitia taarifa rasmi, Apple imeeleza kuwa uamuzi huo umechochewa na dhamira ya kutoa muda zaidi kwa timu zake za maendeleo kuboresha teknolojia mpya itakayofanya iPhone 18 kuwa tofauti kabisa na matoleo yaliyotangulia.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, mabadiliko hayo yanahusisha ubunifu mkubwa katika muundo, kamera, na teknolojia ya akili bandia (AI) ambayo inatarajiwa kuwa sehemu kuu ya mfumo wa iOS mpya.

Taarifa hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki wa Apple duniani, wengi wakionyesha hamu ya kujua ni mageuzi gani makubwa kampuni hiyo inapanga kuleta baada ya kuchukua muda wa ziada.

Kwa sasa, Apple inaendelea na mauzo ya iPhone 17, huku ikiahidi kuwa iPhone 18 itakuwa hatua kubwa ya kihistoria katika mageuzi ya simu janja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *