Tech news

Apple Yatangaza Kufuta Rasmi App ya Clips Baada ya Kukosa Umaarufu Sokoni

Apple Yatangaza Kufuta Rasmi App ya Clips Baada ya Kukosa Umaarufu Sokoni

Kampuni ya Apple imetangaza rasmi kuwa itafuta kabisa app yake ya Clips, ambayo ilizinduliwa mwaka 2017 kwa lengo la kuwasaidia watumiaji wa iPhone na iPad kutengeneza video fupi kwa ajili ya mitandao ya kijamii kama Instagram, Snapchat, na Facebook.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Apple, uamuzi huu umechochewa na ukweli kwamba app hiyo haikupata soko la kutosha, huku watumiaji wengi wakigeukia programu mbadala zinazotoa huduma pana zaidi kama vile CapCut, InShot, VN, na Final Cut Pro.

Clips, ambayo ilitolewa kama suluhisho la haraka kwa wale wanaopenda kuhariri video kwa urahisi kwenye simu au iPad, ilionekana kushindwa kuvutia umati mkubwa wa watumiaji. Licha ya kuwa bidhaa rasmi ya Apple, app hiyo haikuwahi kupata nafasi kubwa kwenye chati za maarufu za App Store.

Apple haijatoa tarehe rasmi ya kuiondoa kabisa kutoka kwenye App Store, lakini imethibitisha kuwa hakutakuwa na masasisho mapya, na huduma ya app hiyo itaisha rasmi miezi michache ijayo.

Kwa sasa, watumiaji wa iOS wanaohitaji suluhisho la hariri ya video wanashauriwa kutumia apps nyingine zenye uwezo mkubwa zaidi, huku Apple ikielekeza nguvu zake kwenye programu kubwa kama Final Cut Pro for iPad.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *