
Timu ya taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Dunia Qatar 2022 kufuatia kuibutua timu ya taifa ya Croatia bao 3-0 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Lusail Jumanne Disemba 13.
Julian Alvarez amefunga magoli mawili moja likiwa ni juhudi binafsi ikichagizwa na uzembe wa walinzi wa Croatia na kisha maajabu ya Messi yakapelekea bao la tatu.
Sasa Argentina wameingia fainali na watapambana na mshindi kati ya Ufaransa na Morocco ambaye atajulikana siku ya Jumatano.
Argentina wamerudia historia ya mwaka 1990 ambapo walifika fainali ya kombe la dunia licha ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Cameroon kwa bao 1-0.
Mwaka huu Argentina waliingia katika kombe la dunia na kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Saudia Arabia kwa bao 2-1.