Gossip

Arnelisa aanika hadharani meseji za Ben Pol

Arnelisa aanika hadharani meseji za Ben Pol

Mwanadada mjasiriamali kutoka nchini Kenya, Anerlisa ameamua kuweka wazi mapungufu ya Ben Pol, ameachia meseji za msanii huyo wa Bongofleva ambazo alikuwa akimtumia kupitia WhatsApp tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Jumbe hizo ambazo zimeanikwa hadharani na mtandao wa Mpasho, zinaonesha Ben Pol akimkumbusha Anerlisa matukio ya maisha yao na kumueleza hisia zake, akitaka warudiane.

Sakata hili lilianza baada ya Ben Pol kufanya mahojiano na mtangazaji Millard Ayo, ambapo alikaririwa akisema hakuwahi kufurahia ndoa yao na ilikuwa ya mapicha picha tu.

Ni madai ambayo yalikanushwa vikali na Anerlisa ambaye alitumia insta story kumuonya Ben Pol asiongelee masuala ya mahusiano yao mitandaoni, vinginevyo atamuanika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *