
Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Aroma hana furaha kabisa na baadhi ya wasanii nchini humo ambao wanalipa vyombo vya habari kuhujumu muziki wake.
Katika mahojiano na Runinga ya NBS Aroma amesema kuna msanii mmoja wa kike nchini Uganda ambaye anahonga vituo vya redio na runinga sizicheze nyimbo zake.
Hitmaker huyo wa “Yoola” amemtaka msanii huyo ambaye anajaribu kuhujumu muziki wake kukoma mara moja na badala yake aelekeze nguvu zake kwenye ishu ya kuwakuza wasanii chipukizi.
Hii sio mara ya kwanza kwa wasanii wa uganda kutoa malalamiko juu wasanii ambao wanahujumu kazi za wenzao kupitia vyombo vya habari kwani mwaka wa 2021 tuliona wasanii kama Naira Ali, Bruno K, na Lydia Jazmine wakiwasuta vikali wasanii wanaohonga vituo vya redio na runinga kucheza nyimbo zao huku wasanii wengine wakisahaulika.