
Nyota wa muziki nchini Arrow Bwoy amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya Otile Brown kudai kuwa hakufurahishwa na kitendo chake cha kushirikisha wimbo wao ambao haukuwa umekamilika kwenye album yake mpya.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio, Arrow Bwoy amesema yuko tayari kusuluhisha tatizo lililopo kati yake na Otile Brown huku akidai hakuwa na ufahamu kuhusu kutoridhika kwa Otile Brown kwa sababu alijieleza kupitia mitandao ya kijamii na yeye hamfuatilii.
Kulingana na Arrow boy, malumbano hayatamfaidi yeye wala Otile Brown, hivyo usimamizi wake utawasiliana na bosi huyo wa Just In Love ili kutafuta suluhu.
Kauli ya Arrow Boy imekuja baada ya Otile Brown kumsuta vikali kwa hatua yake ya kukwenda kinyume na mkataba wa makubaliano wa kutoachia demo ya wimbo wao wa pamoja huku akisema kwamba kitendo hicho huenda ikamshushia brand yake ya muziki ambapo alienda mbali Zaidi na kumtaka Arrow Boy aundoe wimbo wao kwenye digital platfoms mbali mbali kabla hajachukua hatua kali za kisheria.
Utakumbuka Arrow Boy alimshirikisha Otile Brown kwenye wimbo uitwao Show me ambao unapatikana kwenye Albamu yake mpya iitwayo Focus ambayo ina jumla ya ngoma 14 za moto.