
Msanii wa Kenya, Arrow Bwoy, amekubali changamoto ya pambano la ngumi kutoka kwa Shakib Cham, mume wa sosholaiti Zari Hassan. Hii inajiri siku moja tu baada ya Shakib kupokea kichapo cha mbwa kwa knockout na msanii wa Uganda, Rickman Manrick.
Kupitia ujumbe wake, Arrow Bwoy amemjibu Shakib kwa kejeli, akimtaka ajitayarishe ipasavyo endapo pambano hilo litatimia. Hata hivyo, amemtahadharisha Shakib asije akamleta mkewe Zari kwenye ukumbi wa pambano, akisema huenda akazimia kwa aibu baada ya mume wake kushindwa.
Kauli ya msanii huyo inakuja mara baaada ya Shakib kuwapa wasanii wa Kenya changamoto ya kuingia naye ulingoni kama njia ya kuonesha kuwa bado ana nguvu licha ya kichapo alichopokea Uganda hadi akapoteza fahamu.