
Msanii nyota nchini Arrow Boy ametangaza kuanza kwa ziara yake ya kimuziki mwezi Mei mwaka wa 2022 barani ulaya
Arrow boy ameipa ziara hiyo jina la Focus Album World Tour ambayo itaanza Mei 21, mwaka wa 2022 huko Nues nchini Ujerumani.
Ziara hiyo inatarajiwa kupita kwenye miji mbalimbali ikiwemo Paris,Ufaransa Mei 28, Helsinki, Finland tarehe juni 3, na Zurich, Switzerland Juni 4, mwaka wa 2022.
Focus Album World Tour pia inatarajiwa kuzunguka kwenye miji mbalimbali nchini Ujerumani ikiwemo Berlin juni 5, Sturtgart juni 11 na Bremen juni 18 ila Arrow boy ameahidi kuweka wazi nchini zingine ambazo atafanya tour yake hiyo.