Sports news

Arsenal Watinga Raundi ya Nne Baada ya Kulaza Portsmouth 4-1

Arsenal Watinga Raundi ya Nne Baada ya Kulaza Portsmouth 4-1

Washika Mitutu, Arsenal, wamepiga hatua kubwa katika Kombe la FA baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Portsmouth katika mchezo wa raundi ya tano.

Mashabiki wa Portsmouth walipata furaha ya mapema baada ya Bishop kufunga bao dakika ya 3 na kuipa timu yake uongozi. Hata hivyo, matumaini hayo yalidumu kwa muda mfupi tu, kwani Dozzell alijifunga dakika ya 8 na kuisawazishia Arsenal.

Dakika ya 25, Martinelli alionyesha makali yake kwa kufunga bao la pili na kuipa Arsenal uongozi. Baada ya mapumziko, kijana huyo aliongeza bao la tatu dakika ya 51, kabla ya kukamilisha ‘hat-trick’ yake dakika ya 72 na kuhitimisha ushindi wa kishindo kwa Washika Mitutu.

Matokeo haya yanawaweka Arsenal katika nafasi nzuri ya kuendeleza safari yao ya kutafuta taji la Kombe la FA huku mashabiki wakibaki na matumaini makubwa ya kutwaa kombe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *