Sports news

Arsenal Yakubali Kichapo cha Nyumbani Emirates Dhidi ya Man United

Arsenal Yakubali Kichapo cha Nyumbani Emirates Dhidi ya Man United

Klabu ya Arsenal imekubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Manchester United katika mchezo uliopigwa leo katika dimba la Emirates Stadium.

Arsenal walianza kwa furaha baada ya beki wa United, Lisandro Martinez, kujifunga bao dakika ya 29 na kuwapa wenyeji uongozi wa muda. Hata hivyo, United walirejea mchezoni dakika ya 37 kupitia kwa Bryan Mbeumo aliyesawazisha bao hilo kabla ya mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Patrick Dorgu akiipatia Manchester United bao la pili dakika ya 50, na kuifanya Arsenal kuanza msako wa kusawazisha. Juhudi zao zilifanikiwa dakika ya 84 kupitia kwa Mikel Merino aliyefunga bao la pili kwa upande wa Arsenal.

Lakini furaha ya Arsenal haikudumu kwa muda baada ya Matheus Cunha kufunga United bao la ushindi dakika ya 87, na kuwamaliza kabisa matumaini ya wenyeji kupata pointi nyumbani.

Licha ya kipigo, Arsenal wanasalia kileleni mwa Ligi Kuu England na pointi 50, huku United wakipanda hadi nafasi ya nne wakiwa na pointi 38.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *