Sports news

Arsenal Yaomboleza Kifo Cha Raila Odinga

Arsenal Yaomboleza Kifo Cha Raila Odinga

Klabu ya Arsenal imejiunga na mamilioni ya waombolezaji duniani kote kuomboleza kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Amolo Odinga, ikimtaja kama kiongozi mwenye maono, aliyependa maendeleo na kuhimiza amani.

Kupitia taarifa rasmi, miamba hao wa soka wa Uingereza wametuma salamu za rambirambi kwa taifa la Kenya na familia ya Odinga, wakisema Raila alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa na shabiki wa dhati wa timu hiyo.

Raila alikuwa mashabiki maarufu wa Arsenal, akifuatilia kwa karibu michezo yao na kuhudhuria mechi kadhaa katika uwanja wa Emirates jijini London. Mara yake ya mwisho kushuhudia pambano la Arsenal ilikuwa mwezi Machi mwaka 2022, wakati kikosi hicho kilipomenyana na Liverpool.

Kifo cha Raila Odinga kimezua majonzi makubwa si tu nchini Kenya bali pia duniani kote, huku viongozi, mashirika na mashabiki wa michezo wakitoa salamu za pole kwa familia yake na wananchi wa Kenya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *