Gossip

Asili ya Vera Sidika Yazua Mvutano Mitandaoni

Asili ya Vera Sidika Yazua Mvutano Mitandaoni

Mrembo maarufu mtandaoni Vera Sidika amejipata pabaya mbele ya walimwengu baada ya kudai kuwa watu wengi hudhani anatokea Jamaica au Afrika Kusini kutokana na muonekano wake. Kauli hiyo imeonekana kuwakera baadhi ya mashabiki waliomtaka akubali asili yake kama Mluya kutoka Kakamega badala ya kujipendekeza kwa umma.

Mashabiki wengi walimshauri aache drama zisizo na msingi na kujikita zaidi katika malezi ya watoto wake. Wengine walimkosoa vikali wakidai kwamba anampigia mzazi mwenzie, Brown Mauzo, simu nyakati za usiku licha ya wawili hao kuachana rasmi. Baadhi ya wafuasi walionya kwamba kitendo hicho cha kumsumbua Mauzo huenda kikaathiri ndoa ya sasa ya msanii huyo.

Hata hivyo, bado kuna kundi dogo la mashabiki wanaomtetea, wakisema kuwa umaarufu wa Vera umevuka mipaka ya Kenya na kwamba si jambo la kushangaza mashabiki wa kimataifa kumhusisha na tamaduni za mataifa mengine kutokana na taswira yake ya kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *