
Kocha wa timu ya Gabon Patrice Neveu amethibitisha kuwa nyota wa timu hiyo Pierre-Emerick Aubameyang amerudishwa katika Klabu ya Arsenal kwa ajili ya matibabu zaidi.
Aubameyang alikutwa na COVID-19 mnamo January 6 mwaka huu. Hadi sasa hajacheza mchezo wowote wa AFCON na timu yake ambayo ina pointi 4 ikiwa kundi C na timu za Ghana, Morocco na Comoros.