Entertainment

AVRIL AKANA KUWAHI KUTOKA KIMAPENZI NA DIAMOND PLATNUMZ

AVRIL AKANA KUWAHI KUTOKA KIMAPENZI NA DIAMOND PLATNUMZ

Msaniii Avril amekanusha madai kuwa alikuwa na fursa ya kuchumbiana na Diamond Platinumz lakini akachezea nafasi hiyo.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Avril amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwani uhusiano wake na bosi huyo wa WCB ilikuwa ya kikazi na wala sio wa kimapenzi.

“Sijawahi kupata nafasi ya kutoka kimapenzi na Diamond Platnumz, lakini ni rafiki mzuri sana kwangu. Amekuwa rafiki yangu kwa muda mrefu sasa lakini hatuzungumzi mara kwa mara. Lakini anapokuwa ananipigia simu au mimi nikimpigia kwa ajili ya kutaka msaada wa jambo fulani, huwa tunaelewana.” alisema Avril.

Aidha amepuzilia mbali uvumi unaotembea mtandaoni kuwa amekuwa na mazoea ya kumsikiliza Diamond Platnumz nyimbo zake kabla ya kuingia sokoni kwa kusema kwamba alifanya hivyo mara moja tu na sio vinginevyo.

Utakumbukwa mwaka 2012 Avril alitokea kwenye video ya wimbo wa Diamond Platnumz uitwao “Kesho” kama video vixen kitendo kilichowaaminisha walimwengu kwamba huenda mrembo huyo alikuwa kwenye uhusiano ya kimapenzi na msanii huyo wa Bongofleva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *